Mashimo makubwa ambayo yanaweka alama kwenye barabara nyingi katika mji mkuu wa Uganda yamekuwa gumzo katika mtandao wa Twitter.
Kwa kutumia #KampalaPotholeExhibition, wakazi wamekuwa wakiweka picha za mashimo mengi ya jiji ambayo magari yao hulazimika kuzunguka au kupitia katika barabara hizo mbaya.
Mamlaka ya eneo hilo imekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa mashimo hayo yanafikia mita za mraba 8,500 (91,493 sq ft) katika eneo hilo.
Lakini iliongeza kuwa haikuwa na fedha za kuyarekebisha yote.
Wakati mwandishi na mchora katuni Dkt. Jimmy Spire Ssentongo alipoanzisha kampeni hiyo, hata yeye hangeweza kamwe kufikiria aina ya nyenzo ambazo zingetumika.
"Hilo si shimo! Hilo ni bwawa!" alijibu mtu mmoja aliyeshiriki picha mtandaoni.
Baadhi wamegeuza picha kuwa vibonzo mtandaoni na michoro iliyoongezwa kama vile meli zinazovuka mashimo au watu wanaotulia ufukweni.