Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafungwa watoroka baada ya mvua kuharibu gereza la Nigeria

Wafungwa Watoroka Baada Ya Mvua Kuharibu Gereza La Nigeria Wafungwa watoroka baada ya mvua kuharibu gereza la Nigeria

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wafungwa 100 wametoroka jela karibu na mji mkuu wa Nigeria baada ya mvua kubwa kuharibu sehemu waliyokuwa wakihifadhiwa.

Kwa mujibu wa mamlaka, wafungwa 118 awali walikimbia Gereza la Suleja lakini 10 wamekamatwa.

Msako umeanzishwa ili kuwatafuta wengine. Utambulisho wa wafungwa hao haujabainika kufikia sasa lakini kuna hofu kuwa baadhi yao wanaweza kuwa hatari.

Hata hivyo taarifa kutoka katika gereza hilo ilisema wanafanya kazi na vyombo vingine vya usalama na kwamba watu wanapaswa kuendelea na shughuli zao za kawaida bila hofu yoyote.

"Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama [sisi] kufikia sasa tumefanikiwa wakamata wafungwa 10 waliokuwa wakitoroka na kuwaweka chini ya ulinzi, huku tukiendeleza msako mkali wa kuwakamata wengine," ilisema taarifa kutoka kwa mamlaka ya magereza ya Abuja.

Iliongeza kuwa vituo vingi vya magereza huko Suleja, kilomita 50 kutoka Abuja vilijengwa wakati wa ukoloni na hivyo vimezeeka na ni dhaifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live