Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafungwa kwa kufukua fuvu la mtu

Hukumu Pc Data Wafungwa kwa kufukua fuvu la mtu

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAIA watano wa Nigeria wamehukumiwa kifungo cha miaka 12 kila mmoja, baada ya kutiwa hatiani kwa kufukua fuvu la kichwa cha mtu kwa ajili ya kusaka utajiri.

Walipanga wakishalifukua walipeleke kwa mganga wa jadi aliyewaeleza awali kwamba lilihitajika kwa ajili ya kutambika na kuwapatia utajiri. Wanaume hao walikamatwa wakiwa na fuvu hilo kwenye begi na mahakamani walikiri kosa lao.

Mwendesha mashitaka aliiambia Mahakama kwamba wanaume hao walifukua mwili ambao ulizikwa miaka mitatu iliyopita kwenye makaburi ya Kiislamu kwenye jimbo na Niger lililoko kaskazini-kati.

“Walisema mganga huyo aliwaeleza na kuwaahidi kwamba wote watashirikiana katika utajiri utakaowapata, lakini sharti likawa ni kwamba wakatafute fuvu la kichwa cha mtu,” mwendesha mashitaka aliiambia Mahakama.

Maofisa usalama walifanikiwa kuwakamata vijana hao wenye umri wa kati ya miaka 18 na 28 mapema Septemba walipokuwa wakipeleka ‘mzigo’ kwa mganga husika. Mahakama iliwatia hatiani kwa kula njama na kutenda jinai, wakimiliki fuvu hilo kinyume cha sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live