Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafungwa 2,000 watoroka jela Sierra Leone

Wafungwa Sierra Leone Wafungwa 2,000 watoroka jela Sierra Leone

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makumi ya watu waliuawa huku wafungwa karibu 2,000 wakitoroka jela katika mashambulio ya Jumapili dhidi ya kambi ya jeshi, gereza na maeneo mengine nchini Sierra Leone.

Msemaji wa jeshi la nchi hiyo, Kanali Issa Bangura ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, watu 20 wakiwemo wanajeshi 13 waliuawa katika mashambulio hayo ya Jumapili katika mji mkuu Freetown.

Serikali imesema waliohusika na shambulio hilo ni wanajeshi 'waasi' lakini hali ya mambo tayari imedhibitiwa. Hata hivyo imejizuia kusema iwapo shambulio hilo lilikuwa ni jaribio la mapinduzi ya kijeshi au la.

Hapo jana serikali ilitengua amri ya nchi nzima ya kutotoka nje usiku iliyotangazwa Jumapili huku hali ya utulivu ikirejea. Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio pia ametoa hakikisho kwamba utulivu umerejeshwa katika mji mkuu wa Freetown. Amesema aghalabu ya waliofanya ghasia hizo za juzi Jumapili wametiwa mbaroni.

Baadhi ya mashuhuda awali walizieleza duru za habari kwamba, walisikia milio ya risasi na milipuko katika wilaya ya Wilberforce mjini Freetown, kunakopatikana ghala la silaha pamoja na balozi kadhaa za kigeni. Taharuki ilitanda mjini Freetown siku ya Jumapili

Maafisa wa magareza wameviambia vyombo vya habari kuwa, wafungwa 1,890 walitoroka Gereza Kuu la Pademba Road baada ya watu walioukuwa wamejizatiti kwa silaha kulivamia na kuwafungulia wafungwa hao.

Polisi ya nchi hiyo imewataka wafungwa hao warejee jela, huku ikitoa zawadi kwa watakatoa taarifa kuhusu wafungwa hao au waliohusika na mashambulio hayo ya Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live