Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafungwa 100 watoroka jela baada ya gereza kukumbwa na mafuriko

Nigeria Ms (28).jpeg Wafungwa 100 watoroka jela baada ya gereza kukumbwa na mafuriko

Fri, 26 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wafungwa 100 wametoroka jela karibu na mji mkuu wa Nigeria, Abuja, baada ya mvua kubwa kuvunja kuta za kituo walimokuwa wakihifadhiwa, pamoja na uzio wa pembeni.

Kwa mujibu wa mamlaka husika, wafungwa 118 awali walitoroka kutoka katika Gereza la Suleja lakini 10 wakakamatwa. Msako umeanzishwa ili kuwatafuta wengine.

Majina ya wafungwa hao hayakujulikana mapema lakini kuna hofu kuwa baadhi yao ni 'watu hatari'.

Hata hivyo, taarifa kutoka katika gereza hilo ilisema wanafanya kazi na vyombo vingine vya usalama na kwamba watu wanapaswa kuendelea na shughuli zao za kawaida bila hofu yoyote.

Shirika la hali ya hewa la Nigeria hivi karibuni lilitoa onyo ya mvua kubwa na mafuriko kutokea katika baadhi ya majimbo nchini humo. Miaka miwili iliyopita zaidi ya wafungwa 400 walitoroka kufuatia uvamizi kwenye jela nyingine mjini Abuja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live