Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafuasi wa mapinduzi walifanya maandamano mji mkuu wa Niger

Wafuasi Wa Mapinduzi Walifanya Maandamano Mji Mkuu Wa Niger Wafuasi wa mapinduzi walifanya maandamano mji mkuu wa Niger

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Mamia ya wafuasi wa mapinduzi walikusanyika katika mji mkuu wa Niger Niamey katika maandamano siku ya Jumapili kuonyesha uungaji mkono wao kwa utawala wa kijeshi.

Waandamanaji waliopeperusha bendera za Niger na Urusi walionyesha mshikamano na wanajeshi waliompindua rais wao mteule, Mohamed Bazoum, mwezi uliopita.

Ilifuatia tangazo la Jumamosi na mtawala wa kijeshi, Jenerali Abdourahamane Tchiani, kuonya dhidi ya uingiliaji wowote kutoka nje.

Alitangaza pia mpango wa mpito wa miaka mitatu, na kusema kanuni za mpito zitaamuliwa ndani ya siku 30 katika "mazungumzo" yaliyoandaliwa na viongozi wa mapinduzi.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni muda mfupi baada ya kukutana na ujumbe wa amani kutoka jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi, Ecowas, Jenerali Tchiani alisema nchi hiyo haitaki vita lakini alionya kwamba wanajilinda dhidi ya uingiliaji wowote wa kigeni.

Alikashifu vikwazo vya Ecowas vilivyowekewa nchi hiyo akisema havikulenga kutafuta suluhu bali "kutupiga magoti na kutudhalilisha".

Ilikuwa ni onyesho zaidi la kukaidi baada ya wapatanishi wa Ecowas kufanya mazungumzo ya amani na viongozi wa junta katika juhudi za mwisho za kufikia suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo wa kisiasa.

Ecowas imesema kikosi chake cha kusubiri kiko tayari kuingilia kati ikiwa juhudi za amani za kutatua mgogoro huo hazitafanikiwa.

Chanzo: Bbc