Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafuasi wa chama cha Jacob Zuma wapoteza maisha katika ajali

Zuma123.jpeg Wafuasi wa chama cha Jacob Zuma wapoteza maisha katika ajali

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafuasi sita wa chama cha upinzani cha MK kinachoongozwa na Jacob Zuma nchini Afrika Kusini, wamepoteza maisha kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea siku ya Jumamosi, mashariki mwa nchi hiyo.

Katika taarifa yake, chama hicho cha uMkhonto Wesizwe (MK) Party kimeeleza kusikitishwa na ajali hiyo.

Watu wengine kumi walijeruhiwa na kuwahishwa hospitalini,ilisema taarifa ya chama hicho kilichoasisiwa na Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Ajali hiyo imetokea wakati wafuasi wa chama cha uMkhonto Wesizwe (MK) walipokuwa safarini kuelekea Nkandla katika jimbo la Kwa-Zulu Natal.

Licha ya kuwa na miundo mbinu bora ya barabara barani Afrika, lakini Afrika Kusini inaongoza kwa ajali za barabarani, zinazosababishwa na uzembe wa madereva na ubovu wa magari.

Mapema wiki hii, basi lililokuwa linasafiri kati ya Zimbabwe na Afrika Kusini, lilipinduka na kuua watu 10 na kujeruhi wengine 35, katika jimbo la Limpopo kusini mwa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live