Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafuasi wa Zuma wafanya maombi juani

Zuma Pic Wafuasi wa Zuma wafanya maombi juani

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umati mkubwa wa wafuasi wa Jacob Zuma ulikusanyika katika eneo la wazi katika fukwe iliyopo kusini mwa Durban nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya maombi maalum mara baada ya kiongozi huyo kuachiwa huru kwa sababu za kiafya.

Hatua hii imekuja mara baada ya Mahakama kubadilisha adhabu kwa kiongozi huyo mwenye miaka 79 kufuatia madai ya kudharau Mahakama yaliyopelekea kuhukumiwa kifungo cha miezi 15 gerezani.

Hata hivyo aliachiwa mapema mwezi Septemba, taarifa zinaeleza kuwa tangu aachie huru hajawahi kuonekana hadhari kama ambavyo wafuasi hao wamezoea kumuona kiongozi wao.

Siku ya tukio hilo la maombi alionekana kupitia video iliyorekodiwa ambayo ilioneshwa kwa kuchelewa sana huku kundi kubwa la wafuasi likiwa limeondoka kufuatia kukithiri kwa upepo mkali na jua kuzidi.

"Leo ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote wanaiunga mkono pamoja na maombi haya maalum mlioandaa kwa ajii yangu" Amesema Zuma.

Zuma aliongeza kusema kuwa Mahakama imejitia dosari kwa kuamuru akamatwe pasipo kufanya uchunguzi wa kina juu ya madai ya Ufisadi anayoshitakiwa nayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live