Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafuasi wa Odero wafanya ibada nje ya Mahakama

Odero Mk Wafuasi wa Odero wafanya ibada nje ya Mahakama

Wed, 3 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafuasi wa Muhubiri Ezekiel Odero wa Kanisa la New Life International Mavueni kaunti ya Kilifi, wameamua kufanya ibada nje ya Mahakama ya Shanzu kaunti ya Mombasa wakidai wanamuombea Kiongozi wao.

Kwa mujibu wa baadhi ya wafuasi hao, wamesema wamechukua hatua ikiwa ni sehemu ya harakati za kumuombea Mhubiri huyo ambaye amekamatwa kwa tuhuma ambazo wanasema ni za kusingiziwa.

Mchungaji huyo, (Ezekiel Odero), alikamatwa na Polisi akituhumiwa kwa mauaji ya watu 98 ambao ni waumini wa Kanisa la Good News International Ministry la Mchungaji Paul Mackenzie na kufikishwa Mahakamani hapo.

Odero amekuwa kizuizini kwa zaidi ya wiki moja sasa na jana Mei 2, 2023 kesi hiyo ilitarajia kutajwa tena akihusishwa pia na vifo vingine vilivyotokea katika Kanisa lake baada ya kushawishi waumini wake kutorosha ndugu zao wagonjwa waliokuwa Hospitali na kuwapeleka kwake ili awaombee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: