Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafuasi wa Mackenzie waliookolewa washtakiwa kwa kujaribu kujiua

Mackenzie 2023 06 12 At 9.png Wafuasi wa Mackenzie

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 65 waliookolewa kutoka kwenye msitu wa Shakahola wakiwa kwenye mfungo mkali wamegeuzwa kuwa washukiwa, Waathiriwa hao ambao wanasemekana kuwa Wafuasi wa Mchungaji Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International Church Jijini Kilifi sasa wameshtakiwa kwa kosa la kujaribu kujiua kinyume na Kifungu cha sheria cha 226 kama ilivyoandikwa kwenye ukurasa wa 36 wa Kanuni ya adhabu ya Serikali ya Kenya.

Kwa mujibu wa mashtaka yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa upande wa mashtaka, Washukiwa hao walijaribu kujiua kwa kukataa kula chakula wakiwa katika kituo cha uokoaji.

Washukiwa hao wanadaiwa kugoma kula chakula wakiwa katika kituo cha uokoaji mjini Kilifi kati ya Juni 6 na Juni 10.

Washukiwa hao walifanya vurugu na kukataa kula kabisa huku wakitaka wawekewe utaratibu maalum, mapema hii leo Watu 65 hao wamefikishwa Mahakama ya Sheria ya Shanzu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live