Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafuasi tisa wa ANC wafariki kwa ajali ya basi

Screenshot 20240225 234159 Google Wafuasi tisa wa ANC wafariki kwa ajali ya basi

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Wafuasi tisa wa Chama cha ANC cha Afrika ya Kusini wamefariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye mkutano wa kampeni kupata ajali karibu na mji wa Paulpietersbug.

Taarifa ya Mamlaka ya Usalama Barabarani nchini humo, imeeleza kuwa basi hilo lilipata ajali baada ya kupoteza mwelekeo, likiwa na watu 70 na baadhi yao walijeruhiwa.

Watu wanane walikufa papo hapo na mmoja alifariki baadaye baada ya kufikishwa hospitalini.

Waliopata ajali ni miongoni mwa maelfu ya watu waliokuwa wamehudhuria katika uwanja wa mpira jijini Durban siku ya Jumamosi Februari 24, 2024 katika uzinduzi wa ilani ya uchaguzi ya ANC.

Afrika Kusini inatarajia kufanya uchaguzi wa kitaifa na majimbo Mei 29, 2024.

Chanzo: Dar24