Wakenya wawili wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kujisaidia haja katika mbuga ya wanyama, Nairobi nchini Kenya.
Watuhumiwa walikamatwa na maafisa wa KWS waliokuwa wakipiga doria mbugani humo mnamo Septemba 30.
Josephat Bogonko na Isaac Simiyu wamefikishwa katika mahakama ya Kibera na kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu Ann Mwangi.
Mahakama hiyo imeelekezwa kuwa wawili hao wamekana kuhusika na kosa hilo baada ya ufafanuzi wao kuashiria kuwa hawajakubali kosa hilo.
Wanatuhumiwa kutekeleza kosa hilo mnamo Septemba 30, majira ya saa 11 jioni katika mbuga hiyo iliyo karibu na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki.