Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi wawili wa kutoa misaada wauwawa Amhara, Ethiopia

Wafanyakazi Wawili Wa Kutoa Misaada Wauwawa Amhara, Ethiopia Wafanyakazi wawili wa kutoa misaada wauwawa Amhara, Ethiopia

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: Voa

Kundi la kutoa misaada la Catholic Relief Services, CRS, nchini Ethiopia limesema Jumatatu kwamba wafanyakazi wake wawili wameuawa katika jimbo la Amhara, huku wimbi la ukosefu wa usalama likishuhudiwa, baada ya serikali kuu kuvunja vikosi vya usalama vya mikoa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, seriaki ya Ethiopia ilivunja vikosi kutoka majimbo yote 11 nchini, na kuviunganisha na vile vya serikali kuu. Kundi la CRS kupitia taarifa limesema kwamba Chuol Tongyik ambaye ni meneja wa usalama, na Amare Kindeya ambaye ni dereva walipigwa risasi na kuuawa wakati wakirejea kambini kutoka mji mkuu wa Addis Ababa Jumapili.

Haijabainika waliotekeleza mauaji hayo, lakini maafisa watatu wa kutoa misaada ambao hawakutaka kutajwa majina wameambia AP kwamba yalitokea karibu na mji wa Kobo, ambako kulikuwa na mapigano kati ya jeshi la serikali na vikosi vya kieneo vya Amhara mwishoni mwa wiki. Zemede Zewdie ambaye ni mwakilishi wa CRS nchini humo amesema kwamba uchungu na mshtuko waliopata kutokana na tukio hilo hauelezeki.

Ameongeza kusema kwamba kundi lake hutoa msaada kwa watu waliopo hatarini zaidi nchi Ethiopia. Kulingana na wakazi, maandamano na vita vya bunduki vilishuhudiwa kwenye miji kadhaa ya Amhara mwishoni mwa wiki, mengine yakiendelea hadi Jumatatu. Waziri mkuu Abiy Ahmed ameapa kuendelea na mpango wa kuvunja vikosi vya mikoa licha ya upinzani mkubwa unaoendelea mkoani Amhara.

Mikoa mingi ya Ethiopia kwa kawaida huwa na vikosi vyake vya kieneo vyenye nguvu, lakini katiba inaruhusu serikali kuu kuchukua udhibiti wa vikosi vyote kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa kitaifa.

Chanzo: Voa