Wafanyakazi katika sekta ya afya pamoja na elimu jijini Johannesburg nchini afrika kusini wameandamana nje ya makao makuu ya jengo la afya na maabara ya taifa ,wakishinikiza kuhakikishiwa usalama dhidi ya ugonjwa covid 19 pamoja na madai ya kifedha .
Maandamano hayo yamekuja baada mapema mwezi huu idara ya afya nchini humo kutoa taarifa kuwa kiasi wafanyakazi 240 wa sekta ya afya wamekufa kwa ugonjwa wa COVID-19 na zaidi ya wafanyakazi 27,000 wamepatwa na maambukizi .
“Tupo kwenye vita dhidi ya waajiri , na vita hii imekuwa mbaya kadri siku zinavyozidi .na kwa bahati mbaya wanaopata athari ni watu wetu wenyewe,” amesema Juda Mpathi, ambaye ni katibu wa tawi Muungano wa wafanyakazi sekta ya afya na elimu ( NEHAWU).
Nae Waziri wa afya nchini humo Zwelini Mkhize amesema kuwa “niko kwenye mazungumzo maalumu na umoja wa wafanyakazi na tunakubaliana kuchukua hatua mathubuti juu ya mambo yote katika sekta ya afya .”
Afrika Kusini imeripoti visa 611,450 vya ugonjwa Covid 19, na vifo 13,159