Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi uwanja wa ndege wa warejesha begi lenye Sh Mil 44.3 kwa mtalii

C37fd4fe 0b9d 4676 8230 Ed33b35755d8 Wafanyakazi uwanja wa ndege wa warejesha begi lenye Sh Mil 44.3 kwa mtalii

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Wafanyakazi wawili wa uwanja wa ndege wa Kenya na afisa wa polisi wamejizolea sifa baada ya kurudisha begi lililokuwa limebeba takriban $19,000 (Sh Mil 44.3) na vitu vingine vya thamani kwa mtalii wa Uingereza.

Mtalii huyo alikuwa katika kundi ambalo lilikuwa limerejea kutoka safarini katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara alipopoteza begi katika uwanja wa ndege wa Wilson katika mji mkuu, Nairobi.

Wafanyikazi wa uwanja wa ndege na polisi mwanamke walipata begi na kulikagua ikiwa hakuna vilipuzi kabla ya mmiliki kuarifiwa .

"Pesa zote - jumla ya dola 19,000 na baadhi ya maelfu ya shilingi za Kenya zote zilikuwa ziko sawa. Kadi zangu zote zilipatikana zikiwa humo ndani. Vitu vingine vyote vya thamani vilivyojumuisha mavazi niliyopewa na marehemu bibi yangu pia yalikuwa safi. Ilikuwa ndoto yangu ya mchana," Mtalii aliyetambulika kama Benson alisema katika barua pepe ya shukrani kwa polisi wa Kenya.

Alisema alibeba kiasi kikubwa cha fedha ili kufanikisha safari na shughuli za kikundi chake.

Msimamizi wa usalama wa uwanja huo wa ndege, Joseph Kabangi, aliambia runinga ya Citizen ya nchini kuwa "uadilifu ndio thamani kuu" miongoni mwa wafanyikazi katika uwanja huo.

Chanzo: Bbc