Waasi ambao inadaiwa wana uhusiano na kikundi cha Oromo Liberation Army wamelaumiwa kwa kuhusika katika tukio hilo la utekaji wa wafanyakazi zaidi ya 10 wa kiwanda cha simenti kinachomilikiwa na Bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote.
Waasi ambao inadaiwa wana uhusiano na kikundi cha Oromo Liberation Army wamelaumiwa kwa kuhusika katika tukio hilo la utekaji wa wafanyakazi zaidi ya 10 wa kiwanda cha simenti kinachomilikiwa na Bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote. Inadaiwa basi lililokuwa limebeba wafanyakazi hao Wilaya ya Ada'a Berga (kilomita 90 kutoka Mji Mkuu wa Addis Ababa) lilitekwa na hakuna tamko lolote kutoka kikundi cha watekaji ambacho kimekuwa kikifanya matukio hayo kisha kuomba fedha ili kuwaachia mateka.