Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyabiashara Tanzania kuingia Kenya bila vibali

57286ca398868202e7751f07d3e036a0 Wafanyabiashara Tanzania kuingia Kenya bila vibali

Wed, 5 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyata ameruhusu wafanyabiashara kutoka Tanzania kuingia nchini humo bila visa ya biashara wala vibali vya kazi huku akitoa wiki mbili kwa mawaziri wake kushugulikia mlundikano wa malori mipakani mwa nchi hizo.

Kenyatta ametoa kauli hiyo leo katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya lenye lengo la kufungua ukurasa mpya katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano katika masuala ya biashara.

“Ulitukumbusha jana kuwa Taifa la Kenya ndio la tano kuwekeza Taifa la Tanzania, Kampuni 580 za Kenya zimewekeza Tanzania, sisi kampuni za Tanzania zilizowekeza Kenya 30 sisi tunataka kuona wawekezaji wengi wa Tanzania waje kufanya kazi zao Kenya, na nataka niseme leo, wawekezaji wa Tanzania mpo huru wa kuja na kufanya biashara.

“Mawaziri wanaohusika muende mkatatue ile foleni iliyopo Taveta, Namanga kama ni cheti cha covid mawaziri wa afya mkae, kama mtu anacheti cha Tanzania kashapimwa basi waingie wafanye biashara zao na kama mfanyabiashara wa Kenya ana cheti naye aruhusiwe afanye biashara,”amesema Kenyatta.

Kauli ya Rais Kenyatta imekuja ikiwa imepita miezi miwili tangu Wakala ya Kilimo na Chakula wa nchi hiyo ilipotoa taarifa kuwa mahindi kutoka Tanzania yana kiwango kikubwa cha sumu kuvu ambayo ni hatari kwa watumiaji.

Aidha, Kenyatta alisema “Tuna nia tukifanya pamoja tutaweza kuinua uchumi wa Tanzania na Kenya, naamini tukingia kwa kasi hii kwa njia ya ushirikiano, ushindi utakuwa ni mlaini sana kwa nchi zote mbili.

Kenyatta ametaka Watanzania na Wakenya kushirikiana kama ndugu kwa lengo la kuinua uchumi wa wanachi wa pande zote mbili badala ya kushindana.

“Hatuna lolote la kushindana sisi, kwa sababu ukiona kama nchi zinashindana, hatutaweza kupata wawekezaji wakubwa ambao watakuja kuweka viwanda vikubwa nchini mwetu, na vijana kupata ajira.

Chanzo: www.habarileo.co.tz