Wafanyabiashara kutoka soko tofauti jijini Nairobi, ikiwa ni pamoja na soko la Gikomba na soko la Nyamakima muda mfupi uliopita wameandamana kupinga kile walichokitaja kuwa kujipenyeza kwa wauzaji reja reja wa China nchini Kenya.
Wafanyibiashara hao waliandamana hadi afisi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua kudai ulinzi wa biashara zao.
Katika kanda ya video iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii wafanyabiashara hao wanaonekana wakiwa na mabango huku badhi yao waki wikipuliza tarumbeta wakitembea katikati ya jiji la Nairobi.
Maandamano hayo yamefanyika siku moja tu kabla ya tarehe ya mkutano uliopangwa kufanyika kati ya Naibu Rais na wafanyabiashara hao wenye lengo la kuzungumzia ongezeko la wafanyabiashara wa kigeni nchini, hasa raia wa China na Pakistan.
Kulingana na Katibu Mwenezi wa Chama cha Waagizaji na Wafanyabiashara Wadogo Anne Nyokabi, mkutano huo utashughulikia 'utekaji' wa wageni wa masoko ya ndani.