Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafahamu Marais watano wa Afrika waliowahi kufungwa jela

Jsdkd Wafahamu Marais watano wa Afrika waliowahi kufungwa jela

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka jana Mahakama nchini Afrika Kusini ilimhukumu kifungo cha miezi 15 jela, aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jacob Zuma.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya kumpata na hatia ya kukaidi agizo la kufika mahakamani baada ya kukosa kufika kwenye kikao cha uchuguzi wa kesi ya ufisadi wakati alipoikuwa Rais.

Zuma aliyejiuzulu mwaka 2018 anaingia kwenye orodha ya idadi ya marais ama viongozi wakuu wa nchi waliowahi kufungwa jela kwa makosa mbalimbali mara baada ya kumaliza muda wao madarakani ama kujizulu wadhifa huo wa urais.

Makosa mengi wanayofungwa nao viongozi wa mataifa mengi yanahusishwa na masuala ya ufisadi, mauaji au matumizi mabaya ya madaraka.

Zaidi ya viongozi wakuu 40 kutoka nchi za Afrika wamewahi kuonja jela kwa sababu mbalimbali zilizohusiana na nafasi ya ama urais, umakamu wa rais ama waziri mkuu.

BBC inakuletea orodha ya marais watano kutoka Afrika wanaotumikia na waliowahi kutumikia vifungo jela kwa makosa mbalimbali.

1: Omar Al Bashir (Sudan) Aliongoza Sudan kama rais kati yam waka 1989 mpaka 2019, alipoondolewa kwa maandamano ya mwezi April 2019 yaliyosababisha pia vifo vya watu kadhaa.

Al Bashir anatumikia kifungo cha miaka miwili jela kutokana na kukutwa na hatia ya rushwa na kukutwa na mamilioni ya dola kwenye makazi yake.

Kwa mujibu wa sheria za Sudan, mtu mwenye miaka zaidi ya 70, hakai jela ya kawaida, hivyo amefungwa kwenye jela maalumu kwa ajili ya kumrekebisha. Yuko ndani mpaka sasa.

2: Charles Taylor (Liberia) Taylor alikuwa rais wa Liberia kwa miaka sita kati ya mwaka 1997 hadi 2003, yuko jela sasa anaendelea kutumikia kifungo chake cha miaka 50 alichohukumiwa mwaka 2012.

Kesi yake ilichukua zaidi ya miaka mitano kusikilizwa, ilianza kusikilizwa mwaka 2007 wakati huo akiwa na miaka 64.

Taylor alihukumiwa kwa makosa ya dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji, ubakaji na kuweka watu watu wa kingono.

3: Olusegun Obasanjo (Nigeria) Alikuwa Rais wa Nigeria kwa vipindi viwili kati ya mwaka 1976 -1979 na mwaka 1999-2007. Alihukumiwa kwenda jela miaka 30, akimtuhumu aliyekuwa kiongozi wa jeshi la nchi hiyo wakati huo Sani Abacha kama alitumia nguvu za jeshi kumfunga.

Alifungwa miaka 30 jela, lakini baadae ikapunguzwa kwa msamaha wa rais Abacha wakati huo mpaka kufikia 15.

Obasanjo anasema alilipinga jeshi na hasa kiongozi wake, Abacha ndo hasa kilichopelekea kuondolewa madarakani na kuwekwa ndani.

'Msimamo wake ulisababisha nikakamatwa, na kujaribu kunifunga miaka 30 lakini baadae Abacha lipunguza mpaka 15, hata hivyo kwa uwezo wa Mungu nilitumikia miaka mitatu, miezi mitatu na siku tatu tu'.

4: Ahmed Abdallad Mohamed Sambi (Visiwa vya Comoro)

Alishinda kirahisi uchaguzi wa tareh 14 May 2006 na kuwa rais kwenye uchaguzi wa kwanza kidemokrasia usio na machafuko katika historia ya visiwa hivyo.

Alisoma elimu yake yenye misingi ya kiislamu katika nchi za Sudan, Saudi Arabia na Iran, akisoma chii ya Ayatollah Mesbah Yazdi.

Kwa sababu hiyo na kukaa kwake Iran, walimpachika jina la Ayatollah wa Comoros. Lililodumu mpaka leo.

Mwaka 2018 alituhumiwa na kuwekwa ndani kwa makossa yanayohusu hati za kusafiria za visiwa hivyo, akielezwa kupokea hongo ya karibu dola $200,000 kuwezesha hilo kwa kushirikiiana na Bashar Kiwani, mmoja wa wafanyabiashara wakubwa kutoka Syria.

5: Laurent Gbagbo - Ivory Coast Baada ya kuwa mpinzani kwa miaka 20, Lauret Gbagbo alishinda na kuingia madarakani mwaka 2000, miaka miwili baadae kukazuka vita vya wqenyewe kwa wenyewe.

Ghasia hizo zilisababisa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kuhairishwa mara sita mpaka mwaka 2010 ulipofanyika. Hata hivyo alikataa kushindwa katika uchaguzi huo uliompa ushindi Rais Allassane Outtara.

Gbagbo ametoka jela hivi karibuni tu baada ya miaka 10 ya kesi yake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu. Hata hivyo Mahakama hiyo ilimuachia huru miaka miwili iliyopita, baada ya kushindwa kumkuta na hatia licha ya kukaa ndani kwa muda mrefu.

Alishtakiwa na makosa ya uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi zilizosababisha vifo vya wa takribani 3,000 huku zaidi ya watu nusu milioni wakiachwa bila makazi katika uchaguzi uliokubikwa na utata wa 2010.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live