Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waendesha mashtaka waomba adhabu ya kifo watuhumiwa wa "jaribio la mapinduzi" DRC

Waendesha Mashtaka Waomba Adhabu Ya Kifo Watuhumiwa Wa Waendesha mashtaka waomba adhabu ya kifo watuhumiwa wa "jaribio la mapinduzi" DRC

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Waendesha mashtaka wa umma katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wameomba watu 50 wapewe adhabu ya kifo kwa kufanya kile ambacho jeshi linakiita "jaribio la mapinduzi" lililotokea mnamo mwezi Mei.

Mwendesha Mashtaka wa Kijeshi Luteni Kanali Innocent Radjabu alitoa wito huo wakati wa kusikilizwa kwa kesi katika mahakama ya kijeshi ya Kinshasa.

Hata hivyo alimtaka hakimu kumuepusha mshtakiwa mmoja kutokana na adhabu ya kifo, akisisitiza kwamba ana matatizo ya kisaikolojia.

Miongoni mwa washtakiwa wanaokabiliwa na hukumu ya kifo ni Wamarekani watatu.

Mnamo 19, Mei walikuwa sehemu ya kundi lililojihami ambalo lilishambulia nyumba ya aliyekuwa Waziri wa Uchumi Vitale kamerhe, ambaye sasa anahudumu kama mkuu wa Bunge la Kitaifa.

Pia walivamia ofisi ya rais wa nchi hiyo.

Tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo Juni 7, washtakiwa hao wamekuwa wakikabiliwa na mashtaka kuanzia "mashambulizi, ugaidi, kumiliki silaha kinyume cha sheria na zana za kivita, kujaribu kuua, kuua," miongoni mwa mengine.

Upande wa utetezi unatarajiwa kuwasilisha kesi yake siku ya Ijumaa.

Mwezi Machi, serikali ya DRC ilirejesha hukumu ya kifo, na hivyo kusababisha ukosoaji kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu.

Chanzo: Bbc