Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waendesha mashitaka wataka kifungo cha maisha kwa Bunyoni

Bunyoni Burundi.jpeg Waendesha mashitaka wataka kifungo cha maisha kwa Bunyoni

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waendesha mashtaka nchini Burundi wametoa mwito wa kufungwa jela maisha Waziri Mkuu wa zamani Alain-Guillaume Bunyoni

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Burundi anakabiliwa na mashtaka saba, ikiwa ni pamoja na kutumia uchawi kutishia maisha ya rais.

Kesi ya Bw Bunyoni ilianza kusikizwa Septemba, mwaka mmoja baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kumfuta kazi kwa tuhuma za kupanga "mapinduzi" dhidi yake.

Mwendesha Mashtaka Jean-Bosco Bucumi pia anataka Bw Bunyoni alipe "uharibifu sawa na mara mbili ya thamani ya nyumba 153 na viwanja 153 na magari 43 anayomiliki", pamoja na faini ya faranga za Burundi milioni 7.1 ($2,400; 2,000), shirika la habari la AFP liliripoti.

Alain-Guillaume Bunyoni, ambaye alikuwa Waziri Mkuu tangu mwezi Juni 2020, alifutwa kazi mnamo mwezi Septemba 2022, siku chache baada ya rais Evariste Ndayishimiye kushutumu majaribio ya "mapinduzi ya serikali". Nafasi yake ilichukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Gervais Ndirakobuca.

Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi

Kwa muda mrefu Bwana Bunyoni alikuwa akichukuliwa kuwa ndiye kiongozi nambari mbili wa kweli wa utawala na kiongozi wa watu wenye msimamo mkali kati ya majenerali wanaoshikilia madaraka. Alikamatwa mwezi Aprili mwaka huu katika mji mkuu wa kiuchumi Bujumbura, na tangu wakati huo anazuiliwa katika mji mkuu Gitega.

Ndayishimiye alichukua madaraka mwezi Juni mwaka wa 2020 baada ya mtangulizi wake, Pierre Nkurunziza, kufariki dunia kutokana na kile maafisa walisema ni mshtuko wa moyo, licha ya uvumi uliosambaa kwamba aliaga dunia kutokana na Covid 19.

Tangu baada ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoikumba Burundi kati ya mwaka 1993 na 2006 na kusababisha vifo vya watu 300,000, nchi hiyo imekuwa ikidhibitiwa na serikali, kwa msaada wa Imbonerakure, kundi la vijana wa chama tawala, CNDD-FDD, na Idara ya Kitaifa ya Ujasusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live