Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wacongo watolewa Chan

Congo Pic Data Wacongo watolewa Chan

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Ramadhan EliasMore by this Author NCHINI Cameroon jana Jumamosi na leo Jumapili moto  umeendelea kuwaka katika viwanja mbalimbali kunakopigwa mechi za fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) hatua ya robo fainali.

Katika mechi za jana, timu za DR Congo na Congo, zimeondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa na timu pinzani.

DR Congo walicheza na wenyeji Cameroon kwenye hatua hiyo na kufungwa bao 2-1, DR Congo ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Makabi Lilepo aliyefunga kwa kichwa dakika ya 22 bao ambalo lilidumu kwa dakika saba pekee kabla ya Yannick Ndjeng wa Cameroon kusawazisha dakika ya 29 huku dakika ya 42 Felix Oukine Tcheoude akiiandikia bao la pili na la ushindi kwa Cameroon.

Pia Congo nao waliaga mashindanio hayo kama ilivyokuwa kwa majirani zao DR Congo baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi y Mali.

Licha ya kwamba katika mchezo huo uliopigwa kwa dakika 120 hakukuwa na bao, lakini ni moja ya mechi zilizoonesha ushindani mkubwa kwenye hatua hiyo.

Baada ya kufuzu, Cameroon atacheza nusu fainali na mshindi atakayepatikana kwenye mechi kati ya Zambia na Morocco huku Mali akimsubiri mshindi wa mechi kati ya Rwanda na Guinea mechi zitakazopigwa leo Jumapili.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz