Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachungaji wanaswa na sare za jeshi Angola

Wachungaji Wanaswa Na Sare Za Jeshi Angola Wachungaji wanaswa na sare za jeshi Angola

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Wachungaji wawili wa kikundi cha kidini nchini Angola kinachoitwa jeshi la imani, wamekamatwa kwa madai ya kuvaa sare za kijeshi zinazofanana na zile zinazovaliwa na wanajeshi wa jeshi la Angola, vimeripoti vyombo vya habari

Wavuti wa Novo Jornal ulisema kuwa wawili hao walikamatwa Jumatano na maafisa kutoka huduma za upelelezi (SIC) "wakiwa na pini nyekundu sawa na zile zinazovaliwa na majenerali wa jeshi ".

Msemaji wa SIC Manuel Halaiwa amenukuliwa akisema wachungaji hao watashitakiwa kwa matumizi ya sare za kijeshi kinyume cha sheria na kuendesha shughuli haramu za kidini "kwasababu kikundi chao cha kiimani hakijasajiriwa".

Kukamatwa kwao kunafuatia video iliyosambazwa sana ambayo inaonyesha wachungaji hao wawili wakiongoza hafla iliyohudhuriwa na vijana zaidi ya 80 – baadhi yao wakiwa wamevaa magwanda yanayofanana na sare za jeshi.

Shirika la habari la Marekani VOA hivi karibuni liliripoti kuwa serikali ilianzisha msako dhidi ya makanisa ambayo hayajasajiriwa na wale wanaodaiwa kufanya miujiza.

Chanzo: Bbc