Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachumba Wapatikana Wamefariki Dunia Nyumbani Mwao

0fgjhs1v6dd22h2d2g Wachumba Wapatikana Wamefariki Dunia Nyumbani Mwao

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Inaaminika kwamba jamaa alimuua mpenzi wake kabla ya kujitoa uhai

- Kulingana na majirani, wawili hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara nyumbani ambapo waliishia kulishana makonde

- Majirani walisem walipata damu ikiwa imetapakaa mlangoni mwao Jumatatu asubuhi na walipochungulia dirishani, walimuona Mumbi akiwa amelala chini

Wakazi wa kijiji cha Marewa katika kaunti ya Murang’a bado wamebaki midomo wazi baada ya wanandoa kupatikana wameaga dunia nyumbani mwao.

Inaaminika kwamba jamaa alimuua mpenzi wake kabla ya kujitoa uhai ripoti ya Citizen Digital ilisema.

Miili ya Francis Mwangi mwenye umri wa miaka 39 na mwenzake Teressiah Mumbi ilipatikana katika nyumba ambayo walikuwa wakiishi pamoja.

Kulingana na majirani, wawili hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara nyumbani ambapo waliishia kulishana makonde nyumbani.

Miili ya wawili hao ilipelekwa katika makafani ya hospitali ya Murang’a huku uchunguzi kuhusiana na kilichotokea ukianzishwa.

Kulingana na Nancy Wanjiku- jirani wa marehemu- walipata damu ikiwa imetapakaa mlangoni mwao Jumatatu asubuhi na walipochungulia dirishani, walimuona Mumbi akiwa amelala chini.

“Tulikuta damu kwa mlango, langoni pia kulikuwa na damu. Tulipochungulia dirishani tulimuona mama akiwa amelala chini. Walikuwa na ugovi kila mara, kila kuchao hapa kulikuwa na vita,” Wanjiku alise.

Babake Mwangi alisema hana habari kilichomuua mwanawe ila alisema alikuwa amemuoa mke mwingine awali.

Kulingana na mjombake Mumbi, familia yake haikuwa inajua kuhusu ndoa yao ambapo alidai kwamba alikuwa ameolewa kwa jamaa mwingine.

“Hii kuoana kwao mimi sijui, sababu huyu msichana vile najua alikuwa ameolewa na mtu mwingine huyu ni kuchukuana tu walee watoto,” mjombake Mumbi Magochi Mwangi alisema.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke