Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wambwaga spika DRC

C76f11946b5e6470c15521e32d9b1d55 Wabunge wambwaga spika DRC

Sat, 12 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SPIKA wa bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jeanine Mabunda ameondolewa katika nafasi yake baada ya wabunge kupiga kura ya maoni kutokana na muswada uliowasilishwa na upande wa upinzani.

Katika kura hiyo iliyopigwa jana, wabunge 281 kati ya wabunge 484 walipiga kura ya ndiyo iliyotosha kumwondoa spika huyo kutoka chama cha Ujenzi wa jamii na Demokrasia (PPRD) cha Rais Mstaafu Joseph Kabila .

Pamoja na chama cha Kabila kuwa na wabunge wengi bado kilishindwa kumlinda spika kutokana na kuwepo kwa msuguano na mpasuko ndani ya chama.

Kutokana na hali hiyo, kinachotarajiwa nchini DRC ni kuona Waziri Mkuu akijiuzulu. Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kushindwa kwa spika kunasababishwa na kitendo cha Kabila kuchagua spika dhaifu.

Vurugu na ghasia zilitokea ndani ya bunge hilo wiki hii wakati ulipowasilishwa muswada wa kura ya maoni na watu kadhaa walijeruhiwa wakati wanaharakati na wabunge walipoanza kurushiana viti na kuharibu samani ndani ya bunge.

Pamoja na yote hayo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini humo wanasema, huenda isiwe rahisi kwa Rais Tshisekedi kufanya mageuzi ya kiuongozi ikizingatiwa kuwa Joseph Kabila ana ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo.

Mzozo wa hivi karibuni wa kisisia nchini Congo umeibuka tena baada ya rais FĂ©lix Tshikedi kutangaza nia yake ya kuvunja bunge .

Chanzo: habarileo.co.tz