Wabunge wa upinzani nchini Uganda hatimaye wamerejea Bungeni na kuanza kushiriki vikao vya Bunge baada ya kususia vikao hivyo kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Hatua ya Wabunge hao wa mrengo wa upinzani inafuatia ombii la Spika wa Bunge Anita Among kuwataka warejeree bungeni huku akimshinikiza Waziri wa Mambo ya ndani na yule wa usalama kuwasilisha taarifa kuhusu watu wanaodaiwa na upinzani kutoweka baada ya kukamatwa na vyombo vya dola.
Spika aliorodhesha suala la wabunge wa upinzani kwa mara ya kwanza kwenye ratiba ya shughuli za bunge na wabunge wa upinzani walipoiona wakakubali kurejea bungeni.
Lakini hii ilikuwa baada ya kutokea vurugu wakati baadhi ya wabunge wa chama tawala cha NRM na wengine wa upinzani kurushiana maneno na kusababisha wana usalama wa bunge kuingilia kati kuidhibiti hali. Anita Among, Spika wa Bunge la Uganda
Jana Waziri wa Mambo ya Ndani Kahinda Otafire, aliwasilisha taarifa bungeni kuitikia hoja zilizowafanya wabunge wa upinzani kuanza kususia vikao.
Wiki iliyopita, Spika wa Bunge la Uganda alitishia kutangaza viti vyawabunge wa upinzani kuwa wazi, endapo wataendelea kususia kushirikki vikao vya Bunge jambo ambalo lingesababisha kuitishwa uchaguzi mdogo.
Wapinzani nchini Uganda wamekuwa wakkkilalalamikia kile wanachokitaja kuwa kutoweka wafuasi wa mrengo wa upionzani wanaokakmatwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo.