Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wa upinzani Uganda wafikishwa mahakamani tuhuma za mauaji

Mauaji Uganda Wabunge wa upinzani Uganda wafikishwa Kortin tuhuma za mauaji

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanasiasa nguli wa upinzani nchini Uganda wamefikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za mauaji waliyoyafanya kwa kushirikiana na kundi la uhalifu linalojulikana kwa jina la Machete-Wielding Gands la nchini humo.

Viongozi hao wametajwa kuwa ni Mbunge kutoka chma cha National Unity Party(NUP) ambao ni Muhammad Ssegirinya na Allan Sewanyana, wote wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Masaka kujibu tuhuma hizo za mauaji.

Hata hivyo, taarifa ya Jeshi la Polisi inaeleza kuwa waliwateka wanakijiji wapatao 30 kutoka kijiji cha Masaka na kuwatesa hadi kufa huku wengi wao wakiwa ni wazee, tukio hilo walilitekeleza kupitia kundi hilo ndani ya miezi miwili iliyopita.

Nae mwanasheria anae wasimamia katika Kesi hii, amesesitiza kuwa wateja wake hawajafanya mauaji hayo, isipokuwa kinachotendeka ni njama na fitna za kisiasa kutoka kwa Rais Kagame.

Aidha Chama wananchotoka wabunge hao, ndicho chama kikuu cha upinzani nchini humo na ndicho kilicho msimamisha mgombea Bob Wine katika uchaguzi mkuu uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live