Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wa upinzani Senegal wakamatwa mzozo wa kuchaguzi

Wabunge Wa Upinzani Senegal Wakamatwa Katika Mzozo Uchaguzi Wabunge wa upinzani Senegal wakamatwa mzozo wa kuchaguzi

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: Voa

Wabunge watatu wa upinzani nchini Senegal wametiwa mbaroni kutokana na mkanganyiko wa uamuzi wa bunge kuahirisha uchaguzi wa rais kwa miezi 10.

Msemaji wa chama cha upinzani kilichovunjwa cha Pastef, El Malick Ndiaye, aliambia shirika la habari la Reuters kwamba wabunge watatu kutoka muungano wa upinzani Yewwi Askan Wi walikamatwa Jumanne.

Siku ya Jumatatu, wabunge waliidhinisha marekebisho ya dakika za mwisho ili kura hiyo ifanyike mwezi Desemba, na kuongeza muda wa mamlaka ya Rais Macky Sall.

Wabunge wengi wa upinzani walikuwa wameondolewa kwa lazima kutoka bungeni baada ya mijadala mikali.

Ucheleweshaji huo umesababisha maandamano makubwa na wasiwasi wa kimataifa kuhusu demokrasia ya Senegal - miongoni mwa demokrasia imara zaidi katika kanda.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani katika taarifa ilisema hatua hiyo "ni kinyume na utamaduni wenye nguvu wa kidemokrasia wa Senegal".

Jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi, Ecowas, imewataka wanasiasa kuanzisha upya kalenda ya uchaguzi kwa mujibu wa katiba.

Chanzo: Voa