Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wa Afrika Kusini wapiga kura kusitisha uhusiano na Israel

Wabunge Wa Afrika Kusini Wapiga Kura Kusitisha Uhusiano Na Israel Wabunge wa Afrika Kusini wapiga kura kusitisha uhusiano na Israel

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Wabunge wa Afrika Kusini wamepiga kura ya kuufunga ubalozi wa Israel mjini Pretoria na kusitisha uhusiano wote wa kidiplomasia.

Chama tawala cha African National Congress - ambacho kinatawala bunge - kimekuwa kikiikosoa Israel kwa muda mrefu na kiliunga mkono hoja hiyo bungeni.

Hoja hiyo ilitoa wito wa kufungwa kwa ubalozi huo na kusitishwa kwa uhusiano hadi Israel itakapokubali kusitisha mapigano na kujitolea kufanya mazungumzo ya lazima.

Ilipitishwa kwa kura 248 dhidi ya 91. Ilifanya hivyo huku baadhi ya wanachama wakipiga kelele "Palestina huru, huru".

Kabla ya upigaji kura nchini Afrika Kusini, Israel ilimwita balozi wake "kwa mashauriano" - hatua ambayo ilisema ilifuatia "taarifa za hivi punde za Afrika Kusini".

Rais Cyril Ramaphosa hivi karibuni aliipeleka Israel kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa uhalifu wa kivita unaoweza kutokea na kuwarudisha wanadiplomasia wa Afrika Kusini kutoka Israel.

Aliongoza mkutano wa kilele wa kundi la nchi za Brics siku ya Jumanne kujadili hali ya Gaza.

Lugha yake ilikuwa butu, akiishutumu Israel kwa kufanya mauaji ya halaiki huko Gaza na pia kukemea kile alichokiita adhabu ya pamoja ya raia wa Palestina.

Israel imesema hatua zake huko Gaza ni za kujilinda na lengo lake ni kuangamiza Hamas.

Chanzo: Bbc