Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge mbaroni kwa kupiga mawe helkopta ya Odinga

Mawe Odinga Helkopta ya Odinga

Sun, 3 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WABUNGE wawili kutoka nchini Kenya wanatarajiwa kuhojiwa na Ofisi ya Mlelezi wa Makosa ya Jinai kutokana na tuhuma za kuipiga mawe helkopta ya Mgombea urais nchini humo kutoka ODM, Raila Odinga.

Wabunge hao Caleb Kositany kutoka Soy na mwenzake wa Kapseret, Oscar Sudi wameeleza kukubali wito wa polisi na kujiwasilisha kwa Ofisi za DCI za Nakuru nchini humo kwa ajili ya kuhojiwa leo tarehe 3 Aprili, 2022.

Aidha, imeelezwa kuwa Spika wa Kaunti ya Uasin Gishu, David Kiplagat naye alikuwa katika afisi za DCI leo asubuhi kuhojiwa kuhusu tukio hilo.

Tukio hilo lilitokea tarehe 1 Aprili mwaka huu katika mazishi ya Mzee Jackson Kibori ambapo Odinga alikwenda kushiriki mazishi hayo yaliyofayika katika shamba la Samitui kaunti ya Uasin Gishu.

Inaelezwa kuwa kulitokea kundi la vijana waliopiga mawe helkopta hiyo ya Rais na kuharibu mifumo ya hewa sambamba na kuvunja vioo vya gari lake.

Aidha, baada ya tukio hilo, mpizani wa Raila katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyka Agosti mwaka huu, Naibu Rais William Ruto alilaani uhalifu huo na kuagiza vyombo vya usalama kuwachukulia hatua wote walioshiriki.

Aidha, wabunge hao ambao wanatajwa kuwa na ukaribu na Ruto wamekanusha kuhusima katika vurugu hizo.

Walisema kuwa wako tayari kuandika taarifa kwa ofisi za DCI ili kuthibitisha hawakuhusika na kisa hicho.

“Tuko tayari kubeba mzigo huo, tupo kwa ajili ya haki, tunahubiri amani siku zote, tunaelekea Nakuru kwenda kusikiliza upuuzi huu, ni upuuzi mtupu, chochote wanachotaka kufanya tuko tayari kwa hilo.

“Kama wanasiasa, tunapaswa kuacha kuajiri wahuni ili kuwasumbua wengine hata kwenye mazishi. Sio Waafrika,” wamesema.

Aidha, wamedai kushangazwa na hatua ya kuhojiwa kwao ilihali vijana waliihusika wanafahamika.   Mmoja wa wabunge hao alidai kuwa aliambatana na Raila saa chache kabla ya mazishi ya Mzee Kibor.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live