Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge kujadili ripoti mashtaka ya mauaji dhidi ya wanajeshi waliozuru Kenya

Wabunge Kujadili Ripoti Mashtaka Ya Mauaji Dhidi Ya Wanajeshi Waliozuru Kenya Wabunge kujadili ripoti mashtaka ya mauaji dhidi ya wanajeshi waliozuru Kenya

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Wabunge wa Kenya wanatazamiwa kujadili ripoti inayopendekeza mashtaka ya mauaji dhidi ya wanajeshi waliozuru Kenya yafunguliwe katika mahakama za nchini humo.

Pendekezo hilo litakalojadiliwa siku ya Jumanne, limo katika ripoti ya timu ya bunge inayopitia mkataba wa ushirikiano wa ulinzi kati ya Kenya na Uingereza.

Inafuatia ghadhabu ya umma baada ya madai kwamba wanajeshi wa Uingereza huenda walihusika katika mauaji ya Agnes Wanjiru - mwanamke Mkenya aliyepatikana amekufa mwaka wa 2012 baada ya kutumia tafrija ya jioni na wanajeshi.

Inafuatia ghadhabu ya umma baada ya madai kwamba wanajeshi wa Uingereza huenda walihusika katika mauaji ya Agnes Wanjiru - mwanamke Mkenya aliyepatikana amekufa mwaka wa 2012 baada ya kuwa katika tafrija ya jioni na wanajeshi.

Jeshi la Uingereza lilishutumiwa kwa kuficha ukweli, kwa mujibu wa ripoti ya Sunday Times, lakini Wizara ya Ulinzi ya Uingereza baadaye ilisema inashirikiana na uchunguzi wa Kenya kuhusu kifo hicho.

Wabunge nchini Kenya walio katika kamati ya ulinzi pia wanapendekeza kwamba wanajeshi wanaozuru walazimike kuhudumia jamii kupitia uwajibikaji wa kijamii wa shirika.

Walikutana na maafisa wa ubalozi wa Uingereza, maafisa kutoka wizara ya ulinzi na mashauri ya kigeni ya Kenya, pamoja na wapelelezi wanaochunguza mauaji ya Bi Wanjiru kabla ya kuandika ripoti hiyo.

Jeshi la Uingereza lina kitengo cha kudumu cha kufaya mazoezi katika mji wa kati wa Nanyuki chini ya makubaliano na serikali ya Kenya.

Chanzo: Bbc