Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge Kenya wavutiwa huduma Muhimbili

Muhimbili Mloganzila Wabunge Kenya wavutiwa huduma Muhimbili

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wabunge wa Jimbo la Kilifi nchini Kenya wametembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kujifunza matibabu bobezi na kujifunza namna Tanzania ilivyopiga hatua katika sekta ya afya.

Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha MNH, Aminiel Eligaesha imesema wabunge hao Peter Samwel Mwarogo akiwa na wajumbe wa Kamati ya Afya ya jimbo hilo wamepata fursa ya kuona mageuzi kupitia huduma, uwekezaji vifaa tiba, uboreshaji miundombinu na utawala.

Naye Mwarongo amesema wamekuja nchini baada ya kusikia maboresho ya huduma, hususani Hospitali ya Taifa Muhimbili, hivyo wamekuja kujifunza mambo mengi mtambuka, ili wakaboreshe sekta ya afya katika jimbo lao.

Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Afya ya jimbo hilo, Edward Zero, amesema wameona mambo mengi ambayo ni chachu kwao kwenda kuyafanyia kazi.

Amesema wamejadiliana na menejimenti ya hospitali kuhusu usimamizi wa hospitali, kusomesha watalaam, ununuzi wa dawa na vifaa tiba, malipo ya huduma kwa makundi mbalimbali.

Pia wameelezwa kuhusu uendeshaji wa mtambo wa kuchoma taka, uendeshaji kliniki za wagonjwa wa kulipia, uwajibikaji wa watumishi, uendeshaji idara ya dharura, radiolojia na masuala mengine mengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live