Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge Kenya sasa wanataka wapewe huduma ya "massage"

0fgjhs77fol9pg8e3 Wabunge Kenya sasa wanataka wapewe huduma ya "massage"

Sun, 15 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Pendekezo hilo ni kwa minajili ya kuhimarisha afya ya wabunge kutokana na kukabiliwa na wakati mgumu wanapotunga sheriaPia wanataka kituo cha afya bungeni kikarabatiwe kulingana na sheria za Wizara ya Afya za kuzuia msambao wa coronaKamati hiyo pia inataka kitengo cha wanawake kiwe na huduma za kurembesha kucha na kutengeneza nyweleWabunge wanatazamiwa kuanza kupata huduma za ukandaji katika majengo ya bunge iwapo ripoti iliyowasilishwa na kamati ya Huduma za Vifaa Hitajika Bungeni itapitishwa.

Kamati hiyo ilisema pendekezo hilo ni kwa minajili ya kuhimarisha afya ya wabunge kutokana na kukabiliwa na wakati mgumu wanapotunga sheria.

Kando na hayo, pia inataka kituo cha afya bungeni kikarabatiwe kulingana na sheria za Wizara ya Afya za kuzuia msambao wa corona.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Nyaribari Masaba, Ezekiel Machogu ilisema kituo hicho pia kinatakiwa kipanuliwe ili kuongeza vyumba vya ukandaji, kinyozi na ususi.

"Kitengo cha wanaume kipanuliwe ili kiwe na vyumba vya kutoa ulimwende na mazoezi ya viungo," ilisoma ripoti hiyo.

Kamati hiyo pia inataka kitengo cha wanawake kiwe na huduma za kurembesha kucha na kutengeneza nywele.

Wafanyakazi wa kituo hicho cha afya watapewa kandarasi ya miaka mitano yenye uwezekano wa kurefusha kulingana na utendakazi iwapo ripot hiyo itapitishwa.

Wakazi wa Kiambu wamzomea UhuruKwingineko, video iliibuka mtandaoni ikionyesha Rais Uhuru Kenyatta akikemewa na wakazi wa Gatundu ambao wanasema hawamtambui.

Kwa mujibu wa video hiyo, Rais alikuwa kwenye msafara akielekea kijijini mwake Ichaweri wkaati aliamua kuwasalimia wakazi katika eneo la kibiashara la Gatundu.

Licha ya kuwa ndio ngome yake ya kisiasa, hakuna umati ambao unajitokeza kumskiza Kenyatta kama vile hushuhudiwa kwa vigogo wa kisiasa.

Baadhi ya wakazi wanaskika wakimfokea Rais huku wakisema wao ni wafuasi wa naibu wake William Ruto.

"Wacha aende, anatusaidia na nani Wacheni aende, sisi ni wa wheelbarrow, hustler nation . . ." walisema huku msafara wa Rais ukiondoka kwa kasi.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke