Arusha. Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) leo Jumatatu Februari 24, 2020 wamevutana kuhusu kanuni wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wa kuongoza kikao cha Bunge hilo linaloendelea na vikao vyake mjini Arusha.
Hali hiyo imejitokeza kutokana na Spika wa Bunge hilo, Martin Ngoga kupata udhuru.
Kwa mujibu wa mkataba wa ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Ibara ya 56 pamoja na kanuni za Bunge zinatoa nafasi ya kuchaguliwa mwenyekiti wa muda katika kipindi ambacho Spika atakua hayupo.
Katibu wa Bunge hilo, Charles Kadonya amesema tukio kama hilo limewahi kufanyika wakati wa Bunge la kwanza na mbunge kutoka Tanzania, Mabere Marando alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa muda katika kipindi ambacho hakuwepo Spika.
Baada ya ufafanuzi huo, wabunge walimpendekeza Leontine Nzeyimana wa Burundi ambaye amewahi kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Afrika Mashariki pamoja na Fatuma Ndagiza wa Rwanda aliyewahi kuwa balozi wa nchi hiyo nchini Tanzania.
Katika kuendeleza hali ya mshikamano na upendo miongoni mwao, Mbunge kutoka Tanzania, Dk Abdullah Makame alipendekeza kusitisha kwa muda ibara ya nne inayotaka kura zipigwe kwa kuinua mikono akidai jambo hilo lingeondoa umoja wao .
Pia Soma
- Lukuvi amuweka ndani mkurugenzi kwa madai ya kuidanganya Serikali ya Tanzania
- Mwanza wajipanga kukabiliana na maambukizi ya Corona
- Wakulima Tanzania waundiwa mkakati wa kuwanufaisha
“Hili ni jambo muhimu sana kuhakikisha tunapeleka hoja ya kuwa na naibu Spika suala hili litatupa nafasi ya kuhakikisha shughuli za Bunge hazikwami. Spika ni binadamu kama sisi ambaye kwa namna moja au nyingine anaweza kupata dharura,” amesema Aden
Katika uchaguzi huo, Fatuma alipata kura 18 huku Nzeyimana akipata kura 27 na kuongoza kikao cha Bunge.