Wengi wa waathiriwa wa moto katika jengo la ghorofa katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini hawawezi kutambuliwa, mtaalamu wa magonjwa wa serikali amesema.
"Tuligundua asubuhi ya leo kuwa kati ya miili 74 ambayo tumekusanya, tuna miili 12 tu ambayo inaweza kutambulika, ambayo inaweza kutazamwa kwa njia ya macho.
Miili 62 kati ya hii imeungua kiasi cha kutoweza kutambuliwa," Thembalethu Mpahlaza, mtaalamu wa magonjwa kutoka huduma ya Gauteng ya uchunguzi wa miili imeviambia vyombo vya habari nchini humo Ijumaa.
Maafisa wa jiji hilo wamesema kuwa inaweza kuchukua muda kufanya tathmini ya alama za vidole na DNA ili kutambua miili hiyo.