Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waathirika mafuriko Libya waendelea kupokea misaada

Libya Yatangaza Hali Ya Dharura Mwaka Mzima Waathirika mafuriko Libya waendelea kupokea misaada

Sun, 24 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya imetangaza leo kuwa, zaidi ya ndege 70 na meli nane za misaada zimewasili nchini humo tangu nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika ilipokumbwa na mafuriko mabaya kabisa katika historia yake.

Timu ya Dharura ya Radiamali ya Haraka iliyoundwa nchini Libya baada ya kutokea kimbunga na mafuriko hayo makubwa, imesema kwenye taarifa yake kwamba, nchi 24 zimeshapeleka misaada yao kwa waathiriwa wa janga hilo la kimaumbile ambalo limeathiri vibaya maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo na hasa hasa miji ya Benghazi, Al-Bayda, Marj, Susa, Shahatt na Derna.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, moja ya nchi hizo 24 imetoa msaada wa Euro milioni 2 kwa ajili ya chakula, madawa, maeneo ya kuhifadhiwa wahanga, huduma za afya na masuala mengine ya dharura.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, nchi nyingine mbili zimeahidi kutoa msaada wa dola milioni tatu ili kutia kasi juhudi za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Libya.

Athari mbaya za mafuriko zinaendelea kushuhudiwa hadi leo nchini Libya

Karibu watu 4,000 wamethitishwa kufariki dunia kutokana na mafuriko yaliyoyakumba maeneo ya mashariki mwa Libya tarehe 10 mwezi huu wa Septemba. Mafuriko hayo yalisababishwa na kimbunga cha Daniel. Zaidi ya watu 40,000 wamekuwa wakimbizi kwenye maeneo mengine huku idadi kubwa nyingine hawajulikani walipo.

Baraza la Sanate la Libya lenye makao yake mjini Tripoli limeitaka jamii ya kimataifa kufanya uchunguzi huru kuhusu mafuriko hayo ya sababu za kutokea kwake.

Siku chache zilizopita pia, serikali ya Libya ilitangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbwa na mafuriko makubwa ya mashariki mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Haidar al-Sayeh, mkuu wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa nchini Libya, alitoa taarifa na kutangaza idadi ya sumu ambazo zimeripotiwa kutokana na matumizi ya maji ya kunywa huko Derna, Libya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live