Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wauwa Kusini Magharibi mwa Rwanda

Waasi Rwanda Kuuawa Waasi wauwa Kusini Magharibi mwa Rwanda

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Rwanda wanasema “majambazi wenye silaha” wanaoshukiwa kuwa “mabaki” yakundi la waasi National Liberation Front wamewapiga risasi na kuwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine sita siku ya Jumamosi.

Shambulio hilo lilitokea mwendo was aa nanesaa za Afrika Masharikikatika eneo la Kitabi kwenye barabara ya Nyamagabe – Rusizi ambayo inapitia msitu wa Nyungwe kusini magharibi mwa Rwanda Rwanda.

Waliojeruhiwa walihamishwa hadi hospitali ya Kigeme na hospitali ya mafunzo ya chuo kikuu huko Butare, kusini mwa nchi.

Polisi wanasema washambuliaji hao walitokea “upande wa pili wa mpaka.”

Msitu wa Nyungwe ni mojawapo ya maeneo ya mpakani na Burundi.

Hapo awali, nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zilibadilishana tuhuma za kuwaunga mkono waasi wanaotaka kupindua serikali.

Kundi la waasi la Rwanda - linalojulikana kwa ufupi wa jina la Kifaransa FLN - bado halijatoa maoni yoyote.

Kundi hilo lilianza kudai mashambulizi dhidi ya Rwanda - ikiwa ni pamoja na kwenye nyadhifa za jeshi - mwaka 2018 na inasema ina kambi huko Nyungwe, jambo ambalo serikali inakanusha.

Taarifa ya polisi inasema "iliingilia kati kwa dakika chache katika tukio hilo."

"Washambuliaji wanafuatiliwa," inaongeza.

Shambulio hilo linakuja wakati nchi hiyo ikiwa mwenyeji wa mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola mjini Kigali kuanzia Jumatatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live