Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wauteka tena mji wa DR Congo katika mapigano mapya

Waasi Wauteka Tena Mji Wa DR Congo Katika Mapigano Mapya Waasi wauteka tena mji wa DR Congo katika mapigano mapya

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapigano yamezuka tena mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya vikosi vinavyounga mkono serikali na waasi wa kundi la M23.

Wakaazi wanasema waasi hao wameuteka mji wa Kitshanga katika jimbo la Kivu Kaskazini tangu Jumamosi.

Watu kadhaa wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi, kituo cha redio cha eneo hilo kiliripoti.

"Waasi wako Kitshanga na tunajaribu kutafuta njia ya kuuteka tena mji," chanzo cha usalama kiliambia shirika la habari la AFP.

Udhibiti wa eneo hilo umebadilika mara kadhaa tangu mwanzo wa mwaka.

Mapigano yalianza tena wiki tatu zilizopita baada ya makubaliano ya miezi sita. Awali eneo hilo lilikuwa likisimamiwa na kikosi cha kimataifa kilichotolewa na majirani wa Kongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live