Kundi la waasi wa M23 la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema kwamba halitaweka chini silaha ili hali hakuna mazungumzo ya moja kwa moja ya kisiasa na serikali ya Kinshasa.
Msemaji wa waasi hao, Lawrence Kanyuka, ametoa taarifa kwenye mtandao wa Twitter baada ya Rais wa Félix Tshisekedi kusema kuwa hakutakuwa na mazungumzo ya kisiasa na waasi.
Bw Tshisekedi alisema kwamba – chini ya makubaliano na mataifa ya kikanda – waasi wa M23 wanatarajiwa kuweka chini silaha kabla ya kurejea katika maisha ya kiraia.
Chini ya mkataba wa amani uliofikiwa, kikundi hicho kimekuwa kikijiondoa kwenye maeneo kiliyokuwa kimeyateka.
Kwa zaidi ya miezi 18 iliyopita, karibu robo tatu ya watu wameyakimbia mapigano mashariki mwa DRC.