Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wa zamani wa FDLR wahukumiwa kifungo cha miaka 5

Waasi Wa Zamani Wa FDLR Wahukumiwa Kifungo Cha Miaka 5 Waasi wa zamani wa FDLR wahukumiwa kifungo cha miaka 5

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Maafisa 6 wa zamani wa kundi la waasi la FDLR nchini Rwanda wamehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela baada ya kupatikana na hatia ya ugaidi.

Mahakama ya uhalifu wa kuvuka mipaka iliyoko mjini Nyanza kusini mwa Rwanda imesema kwamba maafisa hao walishiriki kikamilifu katika harakati za kijeshi kundi la FDLR dhidi ya Rwanda,mashtaka ambayo wao walikanusha.

Wakati hukumu ilipotolewa mahakama imesema kwamba wamepunguziwa adhabu kutokana na kuwa na mwenendo na ushirikiano mzuri na vyombo vya sheria.

Washitakiwa hao sita hawakuwa mahakamani hukumu hiyo ilipotolewa badala yake imetumiwa teknolojia ya video wao wakiwa katika gereza la Mageragere mjini Kigali.

Hakimu amesema kwamba washtakiwa wote 6 wamepatikana na hatia ya kuwa katika kundi la FDLR lililoidhinishwa na umoja wa mataifa kuwa kundi la kigaidi.

Lakini mahakama imefuta mashtaka mengine mawili dhidi yao ambayo ni kuunda kundi la kijeshi na kutaka kuangusha serikali,huku jaji akisema ‘hakuna ushahidi thabiti uliotolewa na mwendesha mashtaka’

Awali mwendesha mashtaka aliomba hukumu ya kifungo cha miaka 25 jela dhidi ya washtakiwa katika kesi hiyo iliyodumu zaidi ya mwaka moja.

Washtakiwa walisema waliingizwa kwa nguvu katika kundi hilo la waasi dhidi ya Rwanda kwa kuwa walikuwa wakimbizi katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo ambako kundi hilo linaendesha harakati zake.

Upande wa mashtaka ulisema baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994 washtakiwa hao ni miongoni mwa maelfu ya wapiganaji waliokuwa askari wa jeshi la taifa wakati huo waliokimbilia katika nchi ya Zaire ambayo sasa ni Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo na kuanzisha mashambulizi dhidi ya Rwanda, likiwemo shambulio baya linalofahamika kama ‘Oracle du Seigneur’ ama ‘mahubiri ya Mungu’ la mwaka 2001 ambalo kwa mjibu wa mwendesha mashtaka lilisababisha madhara na vifo vya watu kadhaa.

Chanzo: Bbc