Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wa TPLF waharibu miundo mbinu ya Afya

WAASI.png Waasi wa TPLF

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali Nchini Ethiopia inawatuhumu Waasi wa TPLF kwa uharibifu wa maelfu ya Vituo vya Afya eneo la Kaskazini mwa Nchi hiyo na kupelekea Watu zaidi ya Milioni 1.9 katika Mikoa ya Amhara na Afar kukosa huduma ya Afya maeneo hayo.

Waziri wa Afya, Lia Tadesse amesema , Waasi wameharibu miundo mbinu ya Afya ikiwa ni Hospitali 20 na Vituo vya Afya vipatavyo 277 huko Amhara. Hata hivyo TPLF bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na tuhuma hizo.

Mnamo Mwezi Agosti mwaka huu, Waziri wa Elimu , Getahun Mekuria alireporti zaidi ya Shule 7,000 Kaskazini mwa Ethiopia ziliharibiwa na waasi ya TPLF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live