Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wa Mali wadai kudhibiti kambi ya Kidal

Waasi Wa Mali Wadai Kudhibiti Kambi Ya Kidal Waasi wa Mali wadai kudhibiti kambi ya Kidal

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Waasi wa Tuareg wa Mali wanasema wameteka kambi katika mji wa kaskazini wa Kidal iliyoachwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, Minusma, ulisema ulimaliza kuwepo kwake Kidal kwa haraka baada ya msafara wake wa mwisho wa walinda amani kukumbwa na mashambulizi mawili ya IED njiani kuelekea Gao, mji mwingine muhimu kaskazini.

Muungano wa Tuareg ulidai ushindi kwenye mitandao ya kijamii, ukisema ulikuwa unadhibiti kambi ya Kidal.

Afisa mmoja wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba waasi waliikalia kambi hiyo mara tu baada ya kuondolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa.

Ilikuwa kambi ya tatu na ya mwisho kuhamishwa na misheni katika eneo la Kidal, ambalo limekumbwa na ghasia za wanajihadi na wanaotaka kujitenga.

Kambi zingine mbili zilikuwa Tessalit na Aguelhok.

Makundi yanayotaka kujitenga, ambayo hapo awali yalikubali kusitisha mapigano na mamlaka, yameanza tena uhasama katika eneo hilo.Wanapinga walinda amani kukabidhi kambi zao kwa jeshi la Mali.

Serikali ya kijeshi ya Mali imekitaka kikosi cha Umoja wa Mataifa kuondoka nchini humo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, ikisema kuwa utume wake wa muongo mmoja dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu umeshindwa.

Chanzo: Bbc