Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wa M23 wawaua 29 DRC

M23 CONGO CONGOOO Waasi wa M23 wawaua 29 DRC

Mon, 25 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la kutetea haki la Human Rights Watch lenye makao yake mjini New York Marekani linasema kundi la waasi wa M23 limewaua watu 29 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndani ya mwezi mmoja uliopita.

Walioshuhudia waliwaeleza kuwa katika tukio moja katika jimbo la Kivu Kaskazini, waasi hao waliwaua watu 17 ambao waliwashuku kuwa walikuwa wamearifu jeshi la Kongo kuhusu misimamo ya M23.

Wengine walisemekana kuuawa katika mashambulizi yaliyofuata katika eneo hilo.

DR Congo imeishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuunga mkono M23 - jambo ambalo Rwanda inakanusha.

Wiki tatu zilizopita, viongozi wa nchi hizo mbili walikubaliana juu ya "kupunguza ghasia" mashariki mwa Kongo.

Kundi la M23 lilijinyakulia umaarufu mwaka 2012, kabla ya kufurushwa katika mashambulizi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na Congo.

LiIianza mapigano tena mwezi Novemba mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live