Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wa M23 washutumu jeshi kwa mauaji ya raia

E634932e 05fa 4bfa 91f5 F0c41fe89b03 Waasi wa M23 washutumu jeshi kwa mauaji ya raia

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Kundi la waasi la M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limelaani "mauaji ya halaiki na mauaji yaliyolengwa" dhidi ya jamii ya Watutsi yanayofanywa na vikosi vya serikali na washirika wake eneo la mashariki.

Lilisema kuwa vikosi vya muungano vya serikali Jumanne "vimevamia ngome zetu huko Bwiza na maeneo yaliyo karibu, kinyume kabisa makubaliano ya usitishaji mapigano ".

Kundi la M23 limesema vikosi vinavyoshirikiana na serikali vimewaua raia wasio na hatia, kuharibu nyumba, kuwapora na kuwachinja ng'ombe wao, na kubainisha kuwa mashambulizi yanayoendelea yamesababisha raia kutoroka makazi yao na kujeruhi wengi.

"Haya yanalenga mauaji ya Watutsi, na wale ambao wamekataa itikadi ya mauaji ya kimbari ya muungano wa serikali ya DR Congo, wakati jumuiya ya kimataifa na ya kitaifa ilisalia kimya, kutoka zama za kabla ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi. nchini Rwanda," ilisema katika taarifa.

Kundi hilo limesema "halitasimama na kutazama" wakati raia wakiuawa, na kuongeza kuwa "iko tayari kuingilia kati na kukomesha mauaji haya ya kutisha".

Jeshi halijatoa kaili yoyote kuhusu madai hayo lakini wiki iliyopita liliwashutumu M23 kwa kuua makumi ya raia katika mji wa Kishishe mashariki mwa nchi, jambo ambalo walikikana.

Kauli ya M23 inakuja baada ya kundi hilo kukubali kujiondoa katika eneo linalokalia kimabavu kufuatia shinikizo la kudumu kutoka kwa serikali na jumuiya ya kimataifa kufuatia maazimio yaliyokubaliwa na wakuu wa nchi wakati wa mkutano wa hivi majuzi katika mji mkuu wa Angola, Luanda.

Zaidi ya vikundi 50 vyenye silaha vya Congo vilivyohudhuria mazungumzo ya amani yaliyokamilika wiki hii jijini Nairobi pia vilitangaza kuwa vimekubali kuweka chini silaha zao.

Chanzo: Bbc