Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wa Cameroon 'wawanyonga' raia wanaoshutumiwa kwa ujasusi

Waasi Wa Cameroon 'wawanyonga' Raia Wanaoshutumiwa Kwa Ujasusi Waasi wa Cameroon 'wawanyonga' raia wanaoshutumiwa kwa ujasusi

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Watu wanaotaka kujitenga nchini Cameroon wanasema wamewanyonga hadharani raia wawili waliotekwa nyara ambao waliwatuhumu kwa kufanya ujasusi wa jeshi.

Msimamizi wa eneo hilo katika kijiji cha Guzang kaskazini-magharibi alisema uchunguzi unaendelea.

Hii inafuatia kutolewa kwa video iliyoonyesha wanaume wawili wakiwa wamekaa barabarani na kisha kuuawa kwa kupigwa risasi kwa karibu.

Wanaotaka kujitenga wamekuwa wakipigana katika maeneo mawili yanayozungumza Kiingereza nchini Cameroon tangu 2017.

Zaidi ya watu 800,000 wametoroka makazi yao.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamelaani wanajeshi wa serikali na watu wanaotaka kujitenga kwa mauaji, ubakaji, mateso na kuchoma nyumba na shule.

Chanzo: Bbc