Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wa Burundi wavamia uwanja wa ndege saa chache kabla ya Rais kuondoka

Burundi Rebeldd Waasi wa Burundi wavamia uwanja wa ndege saa chache kabla ya Rais kuondoka uwanjani hapo

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikundi cha waasi nchini Burundi kimevamia uwanja wa ndege waa Kimataifa uliopo jijini Bunjumbura majira ya usiku saa chache kabla ya Rais wa nchini humo Evariste Ndayishimiye kuondoka uwanjani hapo kuelekea kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Shambulizi hilo linaripotiwa kutosababisha madhara yoyote katika uwanja huo wa ndege, huku mashuhuda ambao wengi wao ni wafanyakazi wa uwanja w andege wanasema kuwa walisikia milio ya risasi katika uwanja huo ila haikuleta madhara yoyote.

Nae msemaji wa jeshi la nchini humo, amesema kuwa hawakupata taarifa kuhusu tukio hilo katika muda muafaka.

Kikundi hicho cha waasi ambacho chemi chemi yake ni Congo kinatajwa kufanya mauaji ya watu wengi tangu mwaka 2015 , na kuwa kiliingia nchini humo mnamo mwaka 2010.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live