Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wa ADF waua watalii wawili wa kigeni, raia wa Uganda

Waasi Wa ADF Waua Watalii Wawili Wa Kigeni, Raia Wa Uganda Waasi wa ADF waua watalii wawili wa kigeni, raia wa Uganda

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Polisi nchini Uganda wamesema wana wasaka wanaoshukiwa kuwa waasi wa Allied Democratic Forces baada ya kuwapiga risasi na kuwaua raia wawili wa kigeni na mmoja wa Uganda katika Bustani ya Queen Elizabeth wilaya ya Kasese, magharibi mwa Uganda.

Msemaji wa polisi Fred Enanga alisema, ‘’tumesajili shambulizi la kioga la kigaidi la watalii wawili wa kigeni na raia mmoja wa Uganda katika mbuga ya Queen Elizabeth.’’

Gazeti la Daily Monitor limeandika, kulingana na taarifa ya polisi waasi hao walichoma moto gari walilokuwa wakitumia hadi likawa majivu.

‘’Jeshi letu lilichukua hatua mara moja baada ya kupata taarifa hizo na wanawasaka wanaoshukiwa kuwa waasi wa kundi la ADF. Rambirambi zetu ni kwa familia za waathiriwa,’’ Enanga alisema.

Chanzo: Bbc