Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi wa ADF wafanya shambulizi la kifo

Adf C46d7b XL Waasi wa ADF wafanya shambulizi la kifo

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Waasi la Allied Democratic Forces – ADF, la nchini Kongo lenye uhusiano na kundi jingine la dola ya kiislamu, limefanya mauaji ya mtu mmoja na kumjeruhi mwingine wakati lilipolishambulia Lori la mizigo katika eneo la magharibi wa Uganda.

Naibu Msemaji wa Jeshi la Uganda – UPDF, Deo Akiiki amesema wapiganaji hao wa ADF walilivamia lori lililokuwa limebeba Vitunguu katika kona ya barabara ya Katojo ya kijiji cha umbali wa kilometa tatu kutoka mpaka wa Kongo.

Rais akanusha kugawa rasilimali kuwapa hifadhi waasiWaasi SPLM –N waibuka Sudan, waongeza hofu ya mapigano

Akiiki amesema mmoja kati ya watu wanne waliokuwa ndani ya gari hilo, alipigwa risasi na kuuliwa, mwingine hawajulikani aliko, na wa tatu alijeruhiwa vibaya huku mwanamke mmoja kutoroka bila majeraha.

Aidha, ameongeza kuwa kwasasa Vikosi vya jeshi la Uganda vinawafuatilia washambuliaji ili kuwadhibiti wasiweze kuleta madhara zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live