Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi kuteka maeneo yaliyoachwa na vikosi vya kanda ya Afrika mashariki, DR Congo

Waasi Kuteka Maeneo Yaliyoachwa Na Vikosi Vya Kanda Ya Afrika Mashariki, DR Congo Waasi kuteka maeneo yaliyoachwa na vikosi vya kanda ya Afrika mashariki, DR Congo

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Waasi wa M23 wamesema watayakalia tena maeneo ambayo yanaachwa na vikosi vya kanda ya Afrika mashariki vilivyoanza kuondoka kwenye misheni yao mashariki mwa DR Congo siku ya Jumapili.

Kikosi cha Kenya cha takriban wanajeshi 300 kilikuwa cha kwanza kuondoka kwenye nyadhifa zao kupitia uwanja wa ndege wa Goma, hii inawadia baada ya mamlaka yao kutoidhinishwa upya na jumuiya ya eneo kwa kukosolewa na serikali ya Kinshasa.

Mwishoni mwa mwaka jana waasi wa M23 walikabidhi maeneo waliyokuwa wameteka katika maeneo ya Rutshuru, Masisi na Nyiragongo katika jimbo la Kivu Kaskazini kwa vikosi vya Burundi, Kenya, Sudan Kusini na Uganda kama ilivyokubaliwa katika mchakato wa amani wa Luanda na Nairobi.

Haijabainika ni lini wanajeshi kutoka nchi nyingine wataanza kuondoka kwenye nyadhifa zao.

Wanajeshi wa Kenya waliikalia Kibumba na Kibati na maeneo mengine kadhaa ya kilomita kadhaa kaskazini kutoka Goma, mji mkuu wa jimbo hilo.

Katika taarifa, waasi wa M23 walisema "watapona na kuchukua maeneo yote" ambayo walikabidhi kwa vikosi vya kikanda mwanzoni mwa mchakato wa amani.

Usitishwaji wa mapigano haukudumu hivyo basi, mapigano mapya yalizuka mapema mwezi uliopita na kusababisha watu wengi kuyahama makazi yao na vifo vya raia.

Rais aliye madarakani wa DRC "alijuta" kwamba uchaguzi mkuu wa tarehe 20 Desemba hautafanyika katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23.

Chanzo: Bbc