Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waasi M23 waua wanajeshi wa DRC

M23 WAASI Waasi M23 waua wanajeshi wa DRC

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanajeshi wawili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliuawa Jumatatu katika makabiliano na waasi wa kundi la M23 huko mashariki mwa nchi.

Kwa mujibu wa taarifa, waasi wa M23 walishambulia kwa makombora kituo cha jeshi huko Kivu Kaskazini, na kuua wanajeshi wawili na kujeruhi wengine watano.

Mapigano hayo yanajiri huku DRC ikimmshtumu jirani yake, Rwanda, kwamba inaunga mkono kundi hilo la M23, tuhuma ambazo Rwanda inazikanusha.

Mapigano hayo yanafuatia uvamizi uliofanywa Jumapili na waasi kwenye kijiji cha mkoa jirani wa Ituri.

Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wa kundi la ADF waliua wakazi na kuchoma moto nyumba katika kijiji cha Otamabere, wamesema shahidi mmoja, kiongozi na shirika la haki za binadamu katika eneo hilo.

Msemaji wa jeshi la Congo Jules Ngongo amethibitisha shambulizi la ADF bila kutoa idadi ya vifo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live